Monday 30 October 2017

Jinsi ya Kuandaa na Kuchoma Mishikaki ya Figo na Maini



Mara nyingi tunapata mishikaki ya kuchoma kutoka kwenye nyama kawaida, leo nakuonyesha jinsi ya kuandaa mishikaki ya nyama za ndani yaani maini na figo. Katika hali ya kawaida wala hauhitaji vitu vingi kufanya maandalizi kwa maana ya viungo bali unahitaji chumvi na pilipili manga. Lakini leo hapa mimi nimetumia viungo zaidi kama ifuatavyo.

MAHITAJI

  • Maini na Figo nusu kwa nusu – 1/2 kg
  • Mchanganyiko wa chumvi na Pilipili manga kijiko 1 cha mezani
  • Punje nne za kitunguu swaumu – twanga
  • Mchanganyiko wa herbs kijiko 1 cha chai
  • Matone mawili ya soy sauce
  • Udaha robo kijiko cha chai
  • Vijiti vya mishikaki
  • Mafuta ya kupikia vijiko 2 vya mezani

JINSI YA KUFANYA MARINATION YA MISHIKAKI

  1. Kwanza katakata maini na figi katika vipande vidogo vidogo saizi ya mishikaki, weka katika bakuli.
  2. Sasa weka viungo vingine vyote vilivyohorozeshwa na uchanganye kisha acha kwa dakika ishirini.
  3. Sasa tunga vipange vya nyama katika vijiti vya mishikaki.
  4. Kisha anza kuchoma katika moto wa mkaa uliopoa kidogo sio mkali sana. Kila upande kwa dakika 2 na baada ya hapo itakuwa tayari kwa kula
  5. Unaweza jiandalia kachumbali au pilipili na ukafurahia zaidi mishikaki yako

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...