Sunday 29 October 2017

Jinsi ya kumwandaa kuku wa kuchoma kwa oven

Related image

Leo katika mapishi hapa Njoo Tupike , twajifunza jinsi ya kumwandaa kuku wa kuchoma kwa oven ( na sio lazima kwa oven hata kwa jiko la kawaida) cha muhimu ni yale maandalizi ( marination)
MAHITAJI
Vegetable oil
Vitunguu swaumu
Kitunguu maji kimoja kidogo / kipande tu
chumvi
Dried Oregano
Tangawizi
Pilipili
Chicken Masala ( Ila mimi katika mapishi yengu ninayo masala special ila wewe waeza tumia aina yoyote)

Image result for Jinsi ya kumwandaa kuku wa kuchoma kwa oven
JINSI YA KUMUANDAA NA KUCHOMA
Kwanza kabisa andaa viungo vyako vya kumuanda kuu.. Twanga tangawizi, kitunguu swaumu, na chumvi kwa pamoja vilainike kabisa. Kisha weka huo mchanganyiko katika bakuli na ongeza kiasi kidogo cha Oregano ( dried oregano, korogoa kisha ongeza vegetable oil na koroga, weka ile chicken masala tayari pia.
Sasa mwanda kuku wako kwa kumuosha vizuri na kisha mimina vile viungo na ile chicken masala mchanganye kwa dakika chache kisha iache kwa muda wa dakika 15-30 au zaidi yategemea kama uko na muda. Kwani unapomwacha kwa muda zaidi ile marination yako inaingia vizuri katika kuku wako

Baada ya muda huo basi waweza anza kumchoma kuku wako kwa moto wa taratibu kwa muda usiopungua dakika 45 . Amini nakwambia hapo kuku atakua mtamu.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...