Friday, 27 October 2017
NAMNA YA KUANDAA CHAPATI ZA NAZI NA MAYAI
NAMNA YA KUANDAA CHAPATI ZA NAZI NA MAYAI
MAHITAJI
Unga wa ngano kilo 1
Nazi 2
Mayai 3
Chumvi 1/2 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia fanta 1
Maji kiasi
MAANDALIZI
1: Tia unga wako katika kibeseni, tiachumvi, mayai na mafuta kiasi kisha changanya unga wako ,hakikisha unachanganyika ipasavyo.
2: chuja nazi yako ambayo iko tayari na uanze kuponda unga na tui jepesi na kumallizia tui zito,hakikisha unga wako unakuwa laini ili chapati zako zisiwe ngumu na pia uwe makini usikosee wakati wa kukanda
3 : kata vidonge vya saizi upendayo, kunja kwa mafuta ,kuku nja kwa mafuta ni unasukuma mfano wa chapati yenyewe kisha tia mfuta kiasi na ukunje,hiyo pia husaidia chapati kuwa laini na zenye ladha, utaendelea hivyo kwa zote.
4: kisha anza kusukuma chapati zako, tia kikaango jikoni kikipata moto tia chapati na uiche kama sekunde 30 kisha geuza upande mwingine pia hivyo hivyo na utie mafuta huku ukiegeuza geuza hadi iwe rangi ya brauni, utaendelea hivyo kwa chapate zote.
5: baada ya hapo tia chapati zako katika sahani na zitakuwa tayari kwa kuliwa muda wowote,pia waweza kula kwa mchuzi wa nyama au maharage nk..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...
-
Futari ya Mihogo na Viaz Vitamu Kila kitu unapokifanya kwa mfululizo kwa muda mrefu kinachosha. Hata kupika nako kunachosha,i...
-
MAHITAJI/INGREDIENTS Visheti 1.Unga wa Ngano ¼ Kg ¼ Kg Plain Purpose Flour 2.Maziwa ya maji Kikombe Kidogo 1 1 Small Cup...
-
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...
No comments:
Post a Comment