Monday 30 October 2017

SUPU YA MAKONGORO


MAHITAJI
°Kongoro 1/2 au kl 1
°Njegere mbichi 1/4 kikombe
°Karoti 2
°Maggie kidonge 1
°Hoho 1
°Ndimu 1
°Pilipili 1
°Chumvi kiasi
°Nyanya fresh 1
°Kitunguu saumu
JINSI YA KUANDAA
1 : Osha kongoro lako kisha tia katika sufuria weka kitunguu swaumu na ndimu kiasi Acha yaive
2 : Ukiona yako tayari au yanakaribia kuiva epeua kisha weka katika bakuli na utoe mifupa yote
3 : Rudisha jikoni na utie vifaa vyote ulivyo andaa kwa ajili ya supu yako na uache vichemke kwa muda kidogo.
Baada ya hapo supu yako itakua tayari kwa kuliwa
.pia kumbuka ikiwa una pendelea mifupa haina haja ya kutoa. .

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...