Thursday 19 October 2017

UNAIJUA FRUIT CAKE?? CAKE YA MATUNDA, JE UNAWEZA KUIPIKA???

FRUIT CAKE

 MAHITAJI:

 Unga wa ngano 11/2 cups Almonds powder 1 cup Dried fruits 1 cup (raisins,sultanas,candied peel) 

Cherries 1/2 cup (chopped) Sukari (iliyosagwa) 1/2 cup Siagi 3/4 cup Maziwa 1/4 cup B.powder 1 1/2 tsp 

Mayai 4 Arki Almond zilokatwa za kupambia 

MATAYARISHO

 Changanya unga wako na b.powder na unga wa almond weka pembeni.tia arki kwenye maziwa weka pembeni.saga siagi yako na sukari sana mpaka iwe laini weka yai moja moja huku unaendelea kusaga mpaka ichanganyike vizuri sana tia unga wako kidogo kisha tia maziwa yako yenye arki kisha weka unga 
tena weka tena maziwa saga kidogo(hapa hutakiwi kusaga sana lakini unatakiwa uchanganyike vizuri). 

Tia fruits pamoja na cherries koroga kwa mwiko kidogo mimina kwenye trey uliopaka siagi (ile trey ya rectangle kama ya boflo ) weka vipande vya almond juu kwa kupamba.choma kwenye oven 170° kwa 45min- 60mins mpaka ikauke vizuri.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...