Sunday 29 October 2017

Wali wa bizari na viungo

misosi-wali-bizari-main

Wali wa bizari na viungo
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5158
Kuandaa: dakika 10
Mapishi: dakika 25 Walaji: 2 Ujuzi: Rahisi Gharama: Nafuu
Je unahitaji kula wali wa bizari na viungo tofauti kwa ladha zaidi? Jaribu hiki chakula. Ni wali ulio na viungo vya kuamsha vionjo vyote vya ulimi, uliojaa ladha tamu ya viungo, wali ulioiva vizuri na kuchambuka. Unaweza kuongeza au kupunguza viungo kutokana na jinsi unavyopendelea.

Mahitaji
Mchele ½ kilo
Binzano ya njano kijiko 1 kikubwa
Vitunguu maji 2
Binzari nyembamba kijiko 1 chai
Iliki kijiko 1 kikubwa, twanga ½ na nyingine weka ikiwa nzima
Gram masala ½ kijiko cha chai
Mafuta vijiko 3 vikubwa
Hing kijiko 1 kidogo
Chumvi kijiko 1 kidogo
Mdalasini kijiko 1 kidogo
Tangawizi ya unga kijiko 1 kidogo
Wapi kwa kupata bidhaa?
Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.
Maelekezo
Chakula rahisi kuandaa na chenye utamu wa kipekee. Unaweza kuongeza viungo unavyopenda ili kuongeza ladha ya chakula.

misosi-wali-bizari-main2

Andaa viungo – menya na vitunguu.
Weka mafuta yakipata moto, weka kitunguu maji. Angalia kisiive sana, kisha weka viungo vyote na koroga vizuri. Baada ya dakika 2, weka mchele na chumvi kisha koroga.
Weka maji ya moto kiasi funika, hakikisha mvuke hautoki. Punguza moto uwe mdogo sana.
Baada ya dakika 15, funua chakula, geuza na onja kama wali wa chini umeanza kuiva au umeiva kabisa. Ukiwa umeiva weka vijiko 3 vya maji, funika. Baada ya muda geuza.
Baada ya dakika 5 unaweza kuepua na kujiramba.
Unaweza kula chakula hiki mchana au usiku. Ni chakula muafaka kwa familia, lakini punguza viungo vikali kama kuna watoto wadogo wanaokula pia hiki chakula.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...