Monday 27 November 2017

Mkate wa kukaanga wenye mayai na mdalasini


Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Kijiko 1 cha chakula unga wa ngano
½ kikombe maziwa
¼ kijiko cha chai chumvi
Mayai 2
¼ kijiko cha chai mdalasini
½ kijiko cha chai vanilla
Kijiko 1 cha chai sukari nyeupe
Mkate vipande 6
Siagi na mafuta kwa ajili ya kukaangia
Kwenye bakuli kubwa, weka maziwa, mayai, chumvi na sukari. ongeza maziwa koroga vizuri. Ongeza vanilla, mdalasini naunga wa ngano . Changanya hadi ilainike vizuri
Paka mafuta na siagi kiasi kwenye kikaangia katika moto wa wastani. Loweka mkate kwenye mchanganyiko wa unga na mayai hadi ukolee vizuri. Weka mkate kwenye kwenye kikaango
Pika pande zote mpaka uwe na rangi ya kahawia ila usikauke wala kuungua
Pakua yamoto
Enjoy na maple syrup, matunda, asali, ice cream na kingine chochote utakachopenda

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...