Tuesday, 22 May 2018

JINSI YA KUPIKA BIRIANI YA NYAMA


BIRIANI YA NYAMA 


MAHITAJI 

nyama 1kg Mchele (basmat rice )3/4 kg Viazi 1/2 kg Vitunguu 1kg Plain yogurt (maziwa mgando) 500gm 

Tomato puree 300gm Mafuta 1lt Garlic 2 tbls ( ilosagwa) Tangawizi 1 tbls (ilosagwa) Masala ya biriani (garam masala) 2tbls tangawizi powder 1ts 

Pilipili manga1ts Chumvi kiasi Saffron (zafarani) iroweke kwenye maji kidogo. Orange food colour kiasi

 MATAYARISHO 

Safisha nyama weka kwenye dish halafu weka garlic 1tbls, ginger powder, chumvi na black pepper. 

Weka kwenye jiko bila kuweka maji. Acha ichemke kwa muda halafu weka maji mpaka iive zima moto, bakisha na soup kama kikombe kimoja. 

Kata vitunguu vikaange mpaka viwe vyekundu (kumbuka vitunguu vinaendelea kuiva baada ya kutolewa kwenye mafuta kwahiyo vitoe kabla havijapiga wekundu sana ili visiungue).

 Osha mchele uroweke na maji kisha menya viazi vikate vikubwa vikubwa kisha vikaange kwa yale mafuta ulokaangia vitunguu mpaka viwe vyekundu sana lakini visiungue na weka pembeni. 

Gawa vitunguu sehemu mbili moja weka pembeni na moja weka kwenye dish pamoja na yogurt, garlic, ginger, nyanya, mafuta yale ulokaangia vitunguu nusu kikombe na masala ya biriani dish liwe kubwa lenye nafasi (kwa ajili ya nyama na wali baadae). 

Mix pamoja halafu weka kwenye jiko uwe una mix kila wakati ili roast lisiungue. Pika mpaka uhakikishe rangi nyeupe ya yogurt na rangi nyekundu ya tomato pure imeondoka roast limekuwa rangi ya brown. (ukiona mafuta ni mengi ikifika stage hii unaweka kuyapunguza). 

Weka nyama na viazi kwenye roast acha ichemke pamoja, onja chumvi kisha zima moto (roast liwe na maji kidogo sababu ukiweka kwenye oven na wali linakauka). Washa oven moto wa kati.

 Weka maji yawe mengi chumvi na mafuta kijiko 1tbls kwenye dish kubwa weka kwenye jiko acha yachemke. Weka mchele mix kidogo halafu acha uchemke kwa dakika kama 5 utizame uwe umeiva nusu.umwage maji (ukiona unagandana ukoshe kwa maji ya moto). 

Chukua vitunguu vilobaki viweke juu ya roast kisha weka wali wako juu ya vitunguu. Weka zafarani juu ya wali pamoja na rangi ya orange (kama unatumia ya unga itie maji kidogo)funika weka kwenye oven mpaka wali uive

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...