Tuesday, 22 May 2018

Unajua jinsi ys kupika Supu ya nyama na tambi

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 40
Jumla muda; dakika 55

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya viungo vyenye mstari kuona picha ya kiungo



250g/ robo kilo nyama
Karoti 1
Kitunguu 1 cha wastani
Kikombe 1 tambi
Punje 2 kitunguu saumu
Vijiko 2 vya chakula curly leaf parsley (au majani mengine)
½-1 kikombe leek (siyo lazima)
Kijiko 1 chakula beef bouillon powder
Vijiko 2 vya chai mafuta ya mzaituni (olive oil)
Vikombe 3 maji
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Maelekezo

Andaa viungo; katakata karoti, kitunguu maji, leek na curly leaf parsley; twanga kitunguu saumu, weka pembeni



Osha nyama, paka chumvi na pilipili manga (huku kwetu nyama ya supu ina mafuta, kama hupendi mafuta tumia nyama isiyo na mafuta)



Kwenye sufuria katika moto wa wastani, chemsha mafuta. Ongeza nyama na kitunguu saumu. Pika mpaka nyama ianze kupata rangi ya kahawia, kama dakika 5



Ongeza kitunguu maji, kaanga kwa dakika 2-3 nyingine, au mpaka kitunguu kilainike



Ongeza karoti, leek na curly leaf parsley. Kaanga dakika 3 nyingine



Ongeza maji vikombe 3 na beef flavor bouillon powder. Pika mpaka ichemke vizuri



Funika sufuria, acha nyama ichemke moto wa chini kwa dakika kama 20, au mpaka ilainike vizuri kabisa



Ongeza tambi, pika kutokana na maelekezo ya pakiti; mara nyingi inakuwaga dakika kama 7 hadi 9



Ongeza maji endapo yatakuwa yamekauka sana. Ongeza na chumvi ikihitajika



Enjoy

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...