Tuesday, 22 May 2018

USIPOKULA VIZURI UTAKULA DAWA


USIPOKULA VIZURI UTAKULA DAWA
Naam; Usipokula vizuri utakula dawa!
Bila shaka unayajua magonjwa mengi sana yanayotokana na ulaji mbaya, ulaji wa vyakula vibaya na ulaji wa vyakula vyenye uchafu. Unajua matege, upungufu wa damu, ukavu macho, matatizo ya mifupa, uzito mkubwa/unene uliozidi, kwashakoo, kiribatumbo, vidonda mdomoni, matatizo ya uzazi, matatizo ya kinga ya mwili, shinikizo la damu (presha), kisukari, upungufu wa nguvu za kiume nk
Matatizo hayo yote pamoja na mengine mengi yanasababishwa au kuchangiwa na ulaji mbaya – aidha kula zaidi au pungufu ya inavyotakiwa.
Na hivyo hivyo richa ya kupata matibabu na dawa nzuri bila kuzingatia ulaji mzuri basi hayo magonjwa hayawezi kupona wala mgonjwa kupata afadhali.
Hakuna mbadala wa hili. Usipokula vizuri ni lazima utapata matatizo kiafya na hatimaye utakula dawa.
mafuta
Zingatia mambo yafuatayo:
  1. Jua mahitaji ya chakula ya mwili wako kulingana na umri wako, jinsia yako, kazi unazofanya, hali ya lishe ya mwili wako na kadhalika
  2. Kula kulingana na mahitaji yako. Usile zaidi wala pungufu ya virutubisho unavyotakiwa kula kila siku
  3. Kuwa makini zaidi na kiasi cha chumvi, sukari na wanga unachokula. Kiasi kikubwa cha hivi ndiyo huchangia magonjwa mengi zaidi
  4. Jua kila chakula kinakupa nini (Protini, Vitamini, Madini, Wanga, Nyuzinyuzi au Mafuta) na kwa kiasi gani kisha balansi ili kuhakikisha unapata virutubisho aina zote kwa uwiano unaotakiwa
  5. Afya yako ni jukumu lako. Usipojikinga jiandae kugharamia matibabu

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...