Monday 25 June 2018

JINSI YA KUTENGENEZA MAZIWA MAZITO NYUMBANI



Ni rahisi sana kutengeneza maziwa mazito nyumbani kwa mahitaji ya vitu viwili tu 
Maziwa ya maji vikombe 2
Sukari nyeupe kikombe 1
MATAYARISHO 
  1. Kwenye pan yamoto tia sukari na maziwa
2.koroga kwa sekunde 30 au dkk 1 
3.wacha yachemke kwa moto wa kiasi
4.uwe unakoroga mara kwa mara (kila baada sekunde 30 au dakika 1 ili maziwa yasigande au kuunguwa 
5.wacha yachemke kwa moto wa kiasi mpaka yawe mazito yanavyotakikana kwa muda wa dakika 20 hadi 25 

6.zima moto wacha yapoe 
7.yapo tayari kutumiwa au yahifanyi kwenye kikopo cha mfuniko 

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...