Thursday 7 June 2018

Mapishi ya nyama ya kusaga




Mahitaji

  •  Nyama ya kusaga kilo 1
  • Vitunguu maji 2
  • Vitunguu saumu 2
  • Tangawizi 1
  • Nyanya 4
  • Mafuta ¼ lita
  • Chumvi kijiko 1 cha chai
  • Karoti 2
  • Pilipili hoho 1
  • Ndimu. 1


Maelekezo

  •  Menya vitunguu na ukate kwenye vipande vyembamba sana
  • Menya na kwangua karoti iwe kama uji
  • Menya pilipili hoho na kisha kata vipande vyembamba
  • Menya nyanya na zikate kawaida
  • Menya, osha na kisha kwangua tangawizi
  • Twanga vitunguu saumu
  • Bandika sufuria ya kupikia jikoni
  • Weka nyama na anza kukoroga ili kuzuia isigandie kwenye sufuria na kuungua
  • Weka kitunguu maji huku ukiendelea kukoroga kwa muda wa dakika 10
  • Weka kitunguu saumu na tangawiizi. Endela kukoroga kwa muda wa dakika 5 zaidi.
  • Weka mafuta kidogo sana ili kufanya viungo viize.
  • Weka pilipili hoho, karoti na kamulia ndimu. Ongeza chumvi kidogo. Endelea kukoroga.
  • Weka nyanya, koroga na funika sufuria na mfuniko kwa muda kama dakika 10.
  • Funua angalia kama imeiva. Unaweza kujiramba.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...