Thursday 7 June 2018

Ndizi mzuzu zilizoiva









Mahitaji

  • Nazi 1
  • Ndizi mzuzu zilivoiva 6
  • Sukari kijiko 1 cha chai
  • Hiliki


Maelekezo

  • Menya ndizi na zikate kwa urefu ili utoe ule uzi mweusi katika kiini cha ndizi. Usitupe maganda.
  • Menya hiliki na kisha zitwange
  • Kuna nazi na uchuje tui zito na jepesi.
  • Katika sufuria ya kupikia, panga maganda ya ndizi mzuzu,vizuri na kisha juu yake panga ndizi kwa ufasaha.
  • Bandika sufuria jikoni na kisha weka tui jepesi. Acha kwenye moto ichemke hadi tui likauke.
  • Nyunyuzia sukari kidogo kwenye ndizi na weka hiliki.
  • Weka tui zito kisha ache lichemke kwa moto mdogo sana hadi tui likauke.
  • Unaweza kuepua na kujiramba.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...