Wednesday, 11 July 2018

JINSI YA kUTENGENEZA MKATE WA UFUTA


Mahitaji
○ Ngano 1/2
○Ufuta 1/4 kikombe
○Tui la nazi zito vikombe 2
○Hiliki ya unga kijiko cha chai 1
○Hamira kijiko 1 cha chakula
○Yai 1
○Chumvi kiasi
○Sukari kijiko cha chai 1
○Mafuta ya kupikia kijiko upawa 1
JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA
1: Changanya unga, hamira, hiliki, yai,chumvi, sukari na nazi koroga hadi uwe uji kisha acha uumuke, ila hakikisha unga wako unakuwa mwepesi
2 : Baada ya kuumuka chukua kikaango tia katika moto ila hakikisha kikaango chako haki unguzi., koroga maji na chumvi kiasi.
3 : Kikaango kikipata moto nyunyiza maji ya chumvi kidogo kisha chota unga kiasi kwa kutumia kijiko upawa Baada ya hapo sambamza vizuri kwa kutumia kikaango kisha tia Ufuta kwa juu.
4 : Ukiona unaanza kukauka fanya kama unafunika kikaango kwenye moto ili upate rangi ya brown
5 :Kisha toa kwenye kikaango kwa kutumia kisu au kijiko kipana. tia katika sahani na upake Mafuta kwa juu na endelea fanya hivyo hadi unga wote uishe .
Baada ya hatua hizo mikate yako itakua tayari kuliwa.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...