Tuesday, 17 July 2018

Supu ya ng´ombe na mbogamboga



Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 45
Muda jumla; lisaa 1

Mahitaji

500g/ nusu kilo nyama ya supu
Karoti 1 kubwa
Kintunguu maji 1 kikubwa
Hoho nusu mara 3 (rangi tofauti; kijani, njano, nyekundu)
Vijiko 2 vya chai beef bouillon powder au beef cubes 2
Viazi 3 vya wastani
½ kijiko cha chai tangawizi ya unga
Chumvi kwa kuonja ikihitajika
Maji lita 1.5

Maelekezo

Osha na katakata nyama vipande vidogovidogo vya kuingia mdomoni

Andaa mbogamboga; katakata viazi, karoti, kitunguu maji na pilipili hoho, weka pembeni
Kwenye sufuria isiyochika chini katika moto wa juu kiasi, weka nyama, kitunguu maji, tangawizi ya unga na beef bouillon powder. (endapo sufuria yako ni ya kushika chini na nyama ni kavu, ongeza mafuta kijiko 1 cha chakula). Kaanga mpaka nyama iwe ya kahawia na kitunguu kiive vizuri kichanganyike na nyama
Ongeza maji lita 1, funika na mfuniko, acha ichemke kwenye moto wa wastani kwa dakika kama 30 au mpaka nyama ilainike. Endapo maji yatakauka kabla nyama ilainike, ongeza maji kiasi
Maji yakikarikia kukauka na nyama ikishalainika vizuri, ongeza viazi na karoti kwenye nyama
Funika tena, pika mpaka maji yakaukie kabisa
Weka hoho, changanya vizuri, kaanga kwa dakika kama 2
Ongeza maji nusu lita au kiasi unachohitaji kwa supu. Funika na mfuniko tena, acha ichemke kwa dakika kama 5; au mpaka supu ianze kuwa nzito. Ongeza na chumvi ikihitajika
Kula ikiwa ya moto
Enjoy

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...