Friday 31 August 2018

Kuku wa giligilani na chovyo ya Asali

Kuku wa giligilani na chovyo ya Asali

Kuku wa giligilani na chovyo ya Asali

Imezoeleka kua nyama huwekewa chumvi na si sukari au asali.Hapa jikoni leo Nyama italiwa na chovyo la asali.Ni chakula ambacho kila mtu hapa jikoni anakipenda.Naamini Utakipenda pia.
001
Mahitaji
  • Kuku kilo 1,chemsha na chumvi na kitunguu swaumu.
Moja:kuku
  • Unga wa ngano vijiko 6 vya chakula
  • Myai matatu
  • Giligiliani Vijiko 2 vya chai.ponda view laini sana
  • Vitunguu maji vijiko 3 vya chakula,kata vipande vidogo sana
  • Pilipili manga ½ kijiko cha chai
  • Maji robo kikombe (tumia kwa awamu)
Mafuta vikombe 3 ,yakukaangia
Mbili:Chovyo
  • Asali ½ kikombe
  • Tangawizi ya unga vijiko 3 vya chai
  • Apple cidr vinegar vijiko 3 vya chakula
Njia
1. chemsha kuku aive na maji yote yakauke,acha apoe
2.katika bakuli kubwa weka mahitaji yote ya namba moja,changanya adi upate uji mzito na laini.
3.Bandika mafuta jikoni yapate moto,yasiwe yamoto sana
  •   Mafuta yakiwa yamoto sana nyama itaungua kabla haijaiva
  •  Mafuta yakiwa yamoto sana ukiweka kuku mafuta huruka na yanaweza kukuunguza
  • Mafuta yakiwa yamoto sana yanafanya kuku ajae hewa na kisha kupasuka na kurusha mafuta
4.chovya kila kipande cha kuku kwenye uji wa ngano kisha kaanga ,hakikisha unaivisha pande zote  nakua na rangi yadhahabu.
5.Toa kwenye mafuta weka kwenye chujio la mafuta ili kudondoshe mafuta,kisha hamisha na weka kwenye sahani iliyotandikwa karatasi safi yajikoni ili kutoa mafuta yaliyobaki.Kuku tayari
Kuandaa Chovyo
1.katika bakuli,weka mahitaji yote ya namba mbili,changanya vizuri ili kupata rojo .Chovyo tayari
 Weka kuku katika sahani na chovyo katika bakuli kisha tenga kwa pamoja. Chovya kipande chakuku kwenye chovyo kisha kula.Unaweza kula na chakula chochote upendacho.hapa jikoni tulikula na karoti zakuchemsha.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...