Monday, 6 August 2018

Seabass wa kuokwa na chips (takeaway)


Hii pia ni moja ya favorite takeaway yangu. Mara nyingi huwaga nikichoka kula vyakula vya kichinese na vya kihindi au nandos huwa napenda kula samaki wa kuokwa katika mgahawa wa kilebanese ninaoupenda. Hapa nili-order samaki wa kuokwa na chips na salad. Huu ni mlo mzuri wa afya isipokuwa chips tu. Kama ukitaka kuoka samaki mzima kama huyu, muhimu tu kumkata miraba kila upande na kum-marinate masaa matatu hadi sita ili aingie viuungo vizuri na kumuoka kila upande dakika kumi katika moto usiokuwa mkali sana.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...