Sunday 30 September 2018

JIFUNZE KUPIKA: Keki ya nanasi



Keki hii ni nzuri na tamu mana radha yake huongezeka kwa vipande vya nanasi ulivyoweka ndani

Kuandaa: dakika 20
Mapishi: dakika 40,

Mahitaji
Nanasi lililoiva vizuri liwe tamu kata slice
Butter nusu kikombe cha chai
Sukari ya brown nusu kikombe
Juice ya nanasi vijiko 4 vya chakula
Unga vikombe 2
Baking powder kijiko 1 na nusu cha chai
Chumvi nusu kijiko cha 1
Sukari nyeupe vikombe 2
Mayai 3
Mdalasini kijiko 1cha chai
Vanila kijiko 1 cha chai
Butter kikombe 1
Maziwa nusu kikombe
Cherries

Maelekezo
Washa jiko, bandika sufuria au chombo utakachopenda kuokea keki  weka butter iyeyeyuke, weka sukari ya brown isambaze juu.
Chukua slice za nanasi vipange juu ya mchanganyiko, chukua cherries weka kwenye nanasi yaani katikati ya kile kipande cha nanasi.
Epua weka pembeni, chukua bakuli weka unga, chumvi, mdalasini na baking powder changanya vizuri weka pembeni.
Chukua bakuli weka butter, weka sukari nyeupe koroga mpaka ilainike kisha ongeza mayai koroga, weka maziwa, vanila na juice ya nanasi.
Koroga kisha weka mchanganyiko ule wenye unga huku ukiendelea kukoroga vichanganyikane vizuri.
Mchanganyiko uwe mzito ila sio sana. Chukua mchanganyiko wenye unga weka kwenye ule wenye butter na nanasi, sambaza vizuri kisha oka kwa dakika 40.
Epua acha ipoe kwa dakika 5, anza kujiramba na familia.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...