Sunday 30 September 2018

Mchuzi wa nazi wa mbuzi



Pishi hili ni rahisi kupiga liko tofauti kidogo na michuzi ya nazi tulioizoea na ladha yake inamfanya mlaji aendelee kula tu na halina viungo vingi vya kukera. mchuzi ni tofauti na michuzi ya nazi tuliozoea ni wakipekee na ni mtamu Sana, unaweza kulia wali chapati au mkate wowote

Kuandaa: dakika 35
Mapishi: dakika 20

Walaji: 5

Mahitaji
Mahitaji

Mdalasini vijiti 3

Hiliki punje 5

mbegu za pilipilimanga 5

Vitunguu 2vikubwa vilivyokatwakatwa vipande

Vitunguu Thom na tangawizi vilivyosagwa vijiko2

Bay leaf 2

Nyama ya mbuzi nusu

Tui la nazi zito vikombe viwili na nusu

Chumvi

Curry powder kijiko cha chai 1

Mafuta au samli vijiko viwili vya chakula

Mvuje majani 5(sio lazima)

Maji kidogo

Maelekezo

JINSI YA KUPIKA

Chukua nyama yako ioshe vizuri ikate kate ukubwa unaopenda weka chumvi curry powder mchanganyiko wa vitunguu Thom kijito kimoja iache nusu saa ikolee viungo,baada ya nusu saa

Chukua karai lako weka hiliki kaanga bila mafuta toa weka pembeni, weka pilipili manga kaanga toa weka mdalasini kaanga toa, weka bay leaf kaanga toa (hakikisha vyote unakaanga bila mafuta yaani unapasha moto tu na weka kimoja utoe ndio ueke chengine na hakikisha huunguzi)

Chukua sufuria lako weka jikoni weka mafuta eka viungo vyako pamoja na majani ya mvuje weka vitunguu maji weka mchanganyiko wa Thom acha kidogo halafu weka nyama yako ichanganye vizuri weka maji kidogo

halafu weka tui lako huku unagoroga, onja chumvi kama kidogo ongeza acha tui lichemke mpka liive Mchuzi wako utakuwa tayari.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...