Tuesday 2 October 2018

JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA BAGIA ZA DENGU NA VIAZI NYUMBANI.


Vipimo

Unga wa dengu - 3 vikombe vikubwa

Chumvi - 1 kijiko cha chai

Mbatata (kiazi) - 1

Maji baridi - 1 glass

Baking powder - 1 cha chai

Kotmiri  iliyokatwakatwa - 4 -5 Miche

Kitunguu maji kilosagwa - 2 kijiko cha supu

Kitunguu saumu(thomu) ilosagwa au ya unga - 1 kijiko cha chai

Mafuta - 500 ml

Namna  Ya  Kutayarisha Na Kupika

Tumia bakuli  lenye nafasi  mimina unga  na  viungo vyote.

Tia maji ukitumia uma au mchapo wa mkono (usotumia umeme) kuvuruga mchanganyo.

Ukisha kuwa laini bila mavimbo, hakikisha si mzito na si uji sana (mwembamba). Menya kiazi na kwaruza kiwe mithili ya tambi kisha tia ndani ya unga vuruga uchanganyike.

Uwache kwa muda wa robo saa (dakika 15) paka 20.

Weka karai  jikoni au sufuria nzito ndogo, tia mafuta na acha yapate moto sawasawa.

Tumia kijiko cha supu kuteka unga  kutia kwenye mafuta , unapotia hakikisha kipimo chako chote kimelenga mahala au sehemu moja bila ya kutapakaza ili uweze kupata  kidonge .

Utaenedelea hivi kwa kujaza karai nafasi yote zikigeuka rangi ya kuiva, unazigeuza upande wa pili paka umalize zikiwiva kwa rangi nzuri.

Tumia sahani ukiwa umetandaza karatasi za jikoni kuweza kuchuja mafuta baada ya  kuchoma. Kisha badilisha kwenye sahani au bakuli nyengine, tayari kuliwa

Kidokezo:

Huliwa kwa chatini ya aina yoyote, na unapochoma ukiona unga haupandi juu basi lazima kuna itilafu.
#mapishi #mapishigram #mapishiyetu

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...