Tuesday 2 October 2018

JINSI YA KUANDAA NA KUPIKA BUNS ZA SUKARI NYUMBANI



Vipimo
Unga - 3 Vikombe vya chai

Maziwa - 1 Kikombe cha chai

Sukari - ¼ Kikombe cha chai
Siagi - ¼ Kikombe cha chai

Chumvi - ½ Kijiko cha supu

Yai - 1

Hamira - 2 ¼ Vijiko vya chai (pakiti 1)
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katika kibakuli changanya sukari na ½ kikombe ya maziwa yaliyo vuguvugu, kisha tia hamira, koroga na iwache dakika 5 hivi.

Halafu tia yai na yale maziwa ½ kikombe yaliyobakia na siagi iliyoyeyushwa.

Katika bakuli jengine, changanya unga na chumvi kisha ongezea ule mchanganyiko wa hamira.

Kisha ukande unga baada ya kuinyunyizia unga ili usishike.

Ukipenda unaulaza unga firijini kuongeza ladha au unafanya viduara kama 16 na kuziweka kwenye trei ya kuchomea iliyopakwa siagi.

Ziache pahali penye joto hadi ziemuuke.

Washa oveni moto wa 350º.

Piga yai na kijiko kimoja cha maziwa, kisha pakiza juu kabla hujachoma.

Vumbika kwenye oveni kwa muda wa dakika 15 au mpaka zibadilike rangi na viweke kwenye sahani na tayari kwa kuliwa. Asante

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...