Monday, 30 October 2017

Jinsi ya Kukaanga Miguu ya Kuku Ukiwekea na Sosi Maalum


Miguu ya kuku wengi wanaichukulia kama sio chakula kifaacho; ila nakwambia ni mitamu sana ukiweza kuipatia. Leo nitakwambia namna ya kuikaanga ila huko mbeleni ntaonyesha namna ya kutengeneza supu kwa miguu ya kuku.
Pishi la kutosha watu 3

MAHITAJI

  • Miguu 9 ya kuku
  • Chumvi kiasi upendacho
  • Nyanya 3 – zikatwe katwe
  • Vitunguu maji 2 – vikatwe katwe
  • Mafuta ya kupikia kiasi 1/4 lita kwa kukaangia
  • Maji ya limao moja
  • Tangawizi ilopondwa Kijiko kimoja cha chai
  • Kitunguu swaumu punje 4 – menya na kuziponda ponda
  • Mchanganyiko wa viungo vya majani (mixed herbs) kijiko kimoja cha chai
  • Pilipili kama wewe ni mpenzi kwa kiasi upendacho

JINSI YA KUANDAA

  1. Hatua ya kwanza ni kuandaa miguu kwa kuisafisha na kuondoa lile ganda gumu katika kucha au kuzikata kabisa. Mara nyingi maji moto hufaa zaidi kusafishia.
  2. Baada ya kuisafisha unaichemsha kidogo ila sio kuiva hadi kuwa laini sana; hivyo weka chombo na maji, chumvi na mixed herbs kidogo wacha ichemke kwa dakika 5. kisha weka kando ingali katika hicho chombo ibaki katika joto.
  3. Sasa tutengeneze ila sauce – Weka chombo katika moto na mafuta kidogo kisha weka kituguu maji na kukiivisha kidogo kisha weka tangawizi na kitunguu swaumu kisha endelea kuivisha vikiwa vinaelekea kuwa na rangi ya kahawia ndipo uweke nyanya na ile mixed herbs pamoja na pilipili kama unatumia. Ivisha nyanya iivie kabisa kabisa ikiwa tayari weka maji ya limao na kuweka kando.
  4. Sasa turudi kwenye ile miguu ya kuku – itoe katika yale maji na ikiwa inachuja maji; weka chombo cha kukaangia motoni na mafuta
  5. Mafuta yakiwa yamepata moto tumbukiza miguu ya kuku na uikaange hadi iwe rangi ya kahawia. Kisha epua
    Hapo pishi lipo lipo tayari sasa katika kuipakua ndipo unachanganya na ile sauce; waweza weka na kachumbari.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...