Thursday, 30 November 2017

JIFUNZE KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI

MAKANGE YA SAMAKI 
MAHITAJI
Kitunguu kimoja
Hoho moja
Karoti moja
Nyanya kubwa 3
Limao/ndimu moja
Pilipili mbuzi 1 au 2
Samaki Mkubwa mmoja - Sato

MATAYARISHO
Hatua ya 1
Samaki wako anakuwa alishaoshwa vizuri ukamtia ndimu,chumvi na kitunguu saumu baadae ukamkaanga akishaiva unamuweka pembeni.

Hatua ya 2
Osha vizuri na ukate kitunguu makubwa makubwa kiasi usawa wa kushuka chini.Kata hoho na nyanya kwa style hiyo pia kuanzia juu kushuka chini zisiwe nyembamba.
Karoti kama unavyoziona kwenye picha usikate duara kata ndefu ndefu.

Hatua ya tatu
Weka frying pan jikoni na mafuta kaanga kitunguu kisiwe brown ila kiive.Weka nyanya halafu zilianza kuiva na kurojeka kiasi weka hoho na karoti vichemke dk 5.Kata pilipili vidogo vidogo weka,chumvi na Limao acha kwa dk kama 3 kisha muweke samaki ndani ya hilo rosti.
Usimgeuze geuze bali vile viungo ndio uvigeuze ki pembeni pembeni kwa dk chache sana hatakiwi arojeke kisha ipua.

Kula na ugali,ndizi za kukaanga,viazi,mihogo,chips n.k

NOTE
Unaweza tumia samaki - sato mbichi pia sio lazima kukaanga.


MAHITAJI 


Kitunguu kimoja Hoho moja Karoti moja Nyanya kubwa 3 Limao/ndimu moja Pilipili mbuzi 1 au 2 Samaki Mkubwa mmoja - Sato 

MATAYARISHO


 Hatua ya 1 Samaki wako anakuwa alishaoshwa vizuri ukamtia ndimu,chumvi na kitunguu saumu baadae ukamkaanga akishaiva unamuweka pembeni. Hatua ya 2 Osha vizuri na ukate kitunguu makubwa makubwa kiasi usawa wa kushuka chini.Kata hoho na nyanya kwa style hiyo pia kuanzia juu kushuka chini zisiwe nyembamba. Karoti kama unavyoziona kwenye picha usikate duara kata ndefu ndefu. Hatua ya tatu Weka frying pan jikoni na mafuta kaanga kitunguu kisiwe brown ila kiive.Weka nyanya halafu zilianza kuiva na kurojeka kiasi weka hoho na karoti vichemke dk 5.Kata pilipili vidogo vidogo weka,chumvi na Limao acha kwa dk kama 3 kisha muweke samaki ndani ya hilo rosti. Usimgeuze geuze bali vile viungo ndio uvigeuze ki pembeni pembeni kwa dk chache sana hatakiwi arojeke kisha ipua. Kula na ugali,ndizi za kukaanga,viazi,mihogo,chips n.k NOTE Unaweza tumia samaki - sato mbichi pia sio lazima kukaanga.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...