Chapati za viazi ni chapati ambazo zinachanganywa na viazi mviringo vilivosagwa na kuchomwa kama chapati za kawaida, mikate hii asili yake ni kutoka ‘india’ inayojulikana kama ‘aloo paratha’ , ni mara yangu ya kwanza kuifanya so nimeamua kufanya simple recipe na matokeo yake nimeyapenda.
MAHITAJI KWA CHAPATI
Unga wa ngano vikombe 2
Samli vijiko 2 vya supu /ghee
Maziwa ya Unga kijiko 1 cha supu / milk powder (sio lazima)
Chumvi kiasi
Maji yabaridi
MAHITAJI KWA VIAZI
Viazi mviringo 3 vya kiasi
Carrot 1 kubwa
Chumvi
Pilipili ya kuwasha kiasi
Bizari nyembamba / cumin powder 1 kijiko 1 cha chakula
Pilipili manga kiasi /black pepper
MATAYARISHO
Menya viazi na carrot vikate kiasi, vikoshe na uvitie kwenye sufuria ,tia maji kiasi na chumvi, weka kwenye moto mpaka viwive vikauke maji
Vikishakauka maji epua tia pilipili manga,pilipili ya kuwasha na bizari nyembamba(uzile) , visage mpaka viwe havina madonge (viwe laini ) vionje chumvi kama ipo sawa weka pembeni.
Chukua bakuli jengine changanya unga wa ngano, maziwa ya unga (kama uko nayo) , chumvi na samli, mpaka uchanganyike, anza kutia maji kidogo kidogo mpaka donge lishikane, ukande unga uwe mlaini,
Unga ugawe madonge kulinganga ukubwa wa chapati unazopenda, madonge 4 mpaka 6
Madonge utakayotoa, gawanya na viazi madonge sawa na ya unga
Chukua donge 1 la unga lisukume kidogo juu yake weka donge 1 la viazi , lifunge donge la unga ndani yake mukiwa muna donge la viazi, weka pembeni
Fanya hivyo mpaka unamaliza zote
Weka pembeni japo dakika 10 hadi 30, anza kusukuma moja moja na uchome kwa moto wa kiasi
Iweke chapati kwenye chuma/pan ikiwiva upande 1 igeuze upande wa pili, ukianza kuwiva upande wa pili tia mafuta au samli kijiko 1 uzungushe kiasi wacha mpaka uwe rangi unayopenda , utoe na endelea na iliyobaki mpaka unamaliza.
- Kwenye viazi unaweza kuweka pilipili ya unga au nzima ukaikata kata, (nimetumia pilipili ya kupika pia naweza kuengeza viungo/spices unazopenda.
No comments:
Post a Comment