NI wiki nyingine tena mpenzi msomaji tunakutana tena katika safu hii ya Mapishi ya Leo ambapo tunajifunza jinsi ya kuandaa kababu za mayai na nyama ya kusaga, ungana nami.
MAHITAJI
- Nyama ya kusaga (kiasi unachotaka)
- Mayai 5
- Vipande vya mikate
- Chumvi kiasi
- Pilipili manga nusu kijiko cha chai
- Pilipili nzima iliyosagwa nusu kijiko cha chai
- Ndimu kipande
- Mafuta ya kupikia
- Mayai 2 ya kuchomea kababu
- Bizari iliyosagwa
- Vitunguu swaumu na tangawizi ya kusaga
JINSI YA KUPIKA
– Chemsha mayai mpaka yaive vizuri na uyamenye
– Chemsha nyama weka ndimu na chumvi.
-Ikikauka ichanganye na viungo vyote mpaka ichanganyike vizuri.
-Weka vipande vya mkate ambavyo unatakiwa uvivuruge kwa kuvishikia kwa maji kidogokidogo
-Vunja yai moja na uchanganye kwenye mchanganyiko wa nyama.
-Fanya mviringo na uweke kishimo cha kuweka yai ulilochemsha.
-Lifunge ndani vizuri yai kwenye nyama lisionekane.
-Piga yai kwenye kibakuli na uchovye mviringo kisha anza kuzikaanga ndani ya mafuta ambayo tayari yana moto.
-Ikiiva itoe na uiweke kwenye chujio kuchuja mafuta na itakuwa tayari kwa kula.
No comments:
Post a Comment