Wali wa bizari ya mchuzi (tumeric powder) nimetumia recipe rahisi na hauna mahitaji mengi , nimeengeza vipande vya kidali cha kuku (chopped breast chicken) na mchanganyiko wa mboga mboga ila unaweza ukawacha usiweke vitu hivyo kama utakua na kitoweyo chengine pembeni
MAHITAJI
Mchele nusu kg
Kidari cha kuku nusu kg
Mchanganyiko wa mboga mboga vikombe 2(kerot, mahindi machanga,maharage machanga,njegere)
Kitunguu maji 1
Tomato fresh 1
Kitunguu saum kijiko 1 cha chakula
Tangawizi mbichi kijiko 1 cha chakula
Bizari ya mchuzi kijiko 1 cha chai
Chumvi
Bizari nyembamba/ya pilau kijiko 1 cha chakula
Pilipili manga kiasi
Mafuta ya kupikia kiasi
MATAYARISHO
1.Kosha mchele roweka kwa dakika kadhaa , umwage maji, uchemshe mpaka uwive kiasi,mwaga maji uweke pembeni
2.Kataka kata kuku,kitunguu maji na tomato
3.Weka sufuria kwenye moto tia mafuta kiasi(vijiko 3 mpaka 5) , yakipata moto kaanga vitunguu maji ,dakika 2 Hadi 3 vilainike kiasi visiwe brown, tia vipande vya kuku, chumvi, kitunguu saum na tangawizi na bizari ya mchuzi, koroga, tia tomato pamoja na chumvi wacha mpaka viwive, (dakika 5)
4.tia mchanganyiko wa mboga mboga , bizari nyembamba,pilipili manga na koroga tena kidogo
5.Tia ule wali ulioupika koroga vizuri kuufanya uingirangi ya bizari wote, (pole pole bila kuuvuruga)
6.Weka moto mdogo mdogo funika kwa dakika 10 Hadi 15 au mpaka uwive na kukauka vizuri ,epua changanya vizuri na upo tayari kula na Enjoy .
Unaweza kuengeza rangi ya manjano mwishoni ukitaka ukolee rangi .
*sio lazima kutia kuku wala mboga mboga kama una kitooyo pembeni