Wali wa nazi na maziwa
Kuandaa: dakika 5
Mapishi: dakika 10
Mapishi: dakika 10
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mahitaji
- Mchele 1/2 kilo
- Nasi ½ kifuu
- Maji 1 lita (kawaida maji ni mara mbili ya mchele)
- Chumvi ½ kijiko kidogo cha chai
- Sour cream (au maziwa ya kawaida ¼ lita)
Maelekezo
- Andaa tui la nazi kwa kutumia maji ya moto.
- Osha mchele, ila usiloweke.
- Bandika mchele jikoni na ongeza chumvi. Acha mchele hadi uanze kuchemka.
- Baada ya kuanza kuchemka, ongeza tui la nazi pamoja na maziwa. Usikoroge. Acha mchanganyiko uive taratibu kwa takribani dakika 10.
- Kabla maji hayajaanza kukauka, ongeza maziwa
Maalum kwa wale wanaotumia rice cooker :
Kama unatumia rice cooker ni rahisi zaidi
kupika sababu unafanya kila kitu mara moja na unasubiri hadi chakula
kiive. Kwenye hatua ya 3. Changanya kila kitu kwa pamoja – mchele, maji
yenye tui la nazi, sour cream au maziwa na chumvi. Acha wali hadi
uchemke na kuiva.
- Pindua chakula ili kiive vizuri. Kama unatumia jiko la mkaa na unapenda kupalilia chakula, ndio wakati umefika sasa.
- Acha chakula hadi kiive kwa dakika 10 au 15.
No comments:
Post a Comment