![[IMG]](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhzf6tZfXZS15mu5vPJVqv28pTBjNh_dAKuBF_dPTBxxqy2TSOEcQ2S_2Xb-dsA8NpGAD8-nK9EUKewyA7msz1X-R9B6xXCgK8Xq9DPLqMEHW2dciN_pO4Y-JS-xM1g2QWLF5Zdu3sL_kTc/s1600/chef+issa+wali+sausage+(13).jpg)
Mahitaji
- 3 vipande vya sausage
- 1 fungu la majani ya vitunguu
- 1 kitunguu kikubwa
- 100 gram njegere
- 500 gram chele basmati
- 5 gram chumvi
- 5 gram pili pili manga
Jinsi ya kupika
- Weka mafuta ya kupikia kwenye kikaango chako kisha weka vitunguu maji na uvikaange.
- Ongezea majani mabichi ya vitunguu na uendelee kukaanga hadi vitoe harufu na sio kuungua au kubadilika rangi.
- Weka mchele na ukaange kwa dakika 3 mpaka 4 kisha weka maji ya wastani yazidi mchele wako kiasi na uendelee kukoroga ili maji yachanganyike na mchele wako.
- Funikia na weka moto wa wastani ili wali wako uive taratibu.
- chukua sausage zako na kata kata vipande vidogo kisha weka juu ya wali wako njegere zilizochemshwa pamoja na vipande vyoote vya soseji.
- Kumbuka kuendelea kukoroga ili kila kitu kichanganyike, pia kama wewe ni mpenzi wa blue band au samli unaweza weka kiasi ili kuongeza ladha na harufu katika wali wako.
- Baada ya dakika 45 wali wako utakua umeiva kama haujaiva basi ongezea maji kidogo na endelea kupika katika moto mdogo.
Nice meal
ReplyDelete