Habarini za leo wasomaji wetu. Natumai muko wazima wa afya.
Leo nitawaelekeza matumizi sahihi ya Mafuta ya Zaituni (Olive Oil). Pia tutaona faida zinazopatikana kutokana na mafuta haya.
ZIFUATAZO NI BAADHI YA FAIDA ZA MAFUTA HAYA:
(1)Hutibu maumivu ya tumbo kwa kunywa kijiko 1 mara 2 kwa siku
kwa muda wa siku 7 hadi siku 11 inshaallah utapona kabisa.
(2)Mafuta ya zaituni hutibu masheitani
kwa kusomea kisomo cha Ruqia, mgonjwa atajipaka mwili mzima mara moja
kwa siku pamoja na kutafuna vitunguu saumu punje tatu wakati wa kulala
kwa muda wa siku arobaini inshaAllah.
(3)Pia kinga ya masheitani wa kijini na wa kibinadamu kwa kujipaka mwili mzima mara moja kwa siku.
(4)Hutibu ugonjwa wa mafua kwa kupaka kwenye mwamba wa pua na ndani ya matundu ya pua mara tatu kwa siku.
(5)Tiba ya vidonda vya tumbo; Matumizi ni kutia vijiko 2 vya chakula katika uji mara mbili kwa siku kwa muda wa siku 90.
(6) Mafuta ya zaituni hutumika kama
huduma ya kwanza kwa aliyekunywa sumu kwa kunywa, na kwa mwenye ganzi au
kiharusi hutumia kwa kuchua mwilini asubuhi na jioni.
(7) Mafuta ya zaituni hutumika katika
kuua wadudu wabaya walioko tumboni kwanjia ya kunywa kijiko kimoja mara
mbili kwa siku kwa muda wa siku saba.
(8) Mafuta ya zaituni huongeza nguvu za
kiume kwa kunywa kijiko kimoja kwa siku pamoja na kuuchua uume mafuta
yaliyochanganywa na vitunguu swaumu kwa muda wa siku saba hadi kumi na
moja.
(9) Tiba ya ugonjwa wa kusahau: paka
katika paji la uso kutwa marambili pamojana kunywa kijiko kimoja cha
chai mara moja kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi siku 11.
(10) Tiba ya degedege: hutumika kupakaa
mwili mzima mafuta yaliosomewa ruqya, marambili kwa siku kwa muda wa
siku 7 hadi siku 21.
(11)Kukojoa kitandani: kupakaa mafuta ya
zaitun mwili mzima kutwa marambili huku akilamba matone mawili kwa muda
wa siku 7 hadi siku 21.
BAADHI YA FAIDA ZENGINE NI KAMA VILE
(12) Husaidia kupunguza mafuta mwilini.Mafuta haya yanajulikana kama kolestero (Cholesterol).
(13) Inapunguza makali ya njaa.
(14) Utumiaji wa mafuta haya unapunguza hatari ya ugonjwa wa moyo (coronary heart disease) hasa kwa wanawake.
(15) Yanasaidia kuzuia kansa ya matiti. Mafuta haya yana phytochemicals ambayo inasaidia kuzuia kansa.
Kwa kweli faida za haya mafuta ni nyingi sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...
-
Futari ya Mihogo na Viaz Vitamu Kila kitu unapokifanya kwa mfululizo kwa muda mrefu kinachosha. Hata kupika nako kunachosha,i...
-
MAHITAJI/INGREDIENTS Visheti 1.Unga wa Ngano ¼ Kg ¼ Kg Plain Purpose Flour 2.Maziwa ya maji Kikombe Kidogo 1 1 Small Cup...
-
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...
No comments:
Post a Comment