Ngano 1/2 kilo mayai 3 mafuta au samli 1/4 kikombe kitunguu kikubwa
kilichosagwa 1 Kitunguu Swaumu punje 4 Chumvi 1/2kijiko au kulingana na
matakwa yako.
NAMNA YA KUANDAA
chapati za maji 1 Chekecha unga wako vizuri weka katika bakuli safi. 2
Tia maji katika bakuli la unga na ukoroge mpaka upate uji wa wastani si
mzito san a wala si mwepesi sana. 3 Ongeza mayai na chunmvi endelea
kukoroga. 4 Ongeza kitunguu swaumu na kitunguu maji. Injika kikaango
chako jikoni subiri kipate moto. 5 Chota pawa moja mimina na tandaza
kuzunguka kikaango subiri sekunde tano hadi kumi mpaka ikauke kisha
geuza upande wa pili. 6 Tia mafuta huku ukigeuza na kuzungusha ili
mafuta yaenee pande zote na ili chapati isiungue. Endelea kugeuza mpaka
iwe rangi ya kahawia. 7 Hapo chapati zitakua tayari kwa kuliwa. 8 Fanya
hivyo kwa chapati zote zilizobakia Matayarisho hayo yanatosha kupika
chapati za mayai/laini sita (6) mpaka kumi (10) . Chapati za maji
hupendeza zaidi kuliwa Michuzi mizito, Chai na kadhalika. Nenda kajaribu
kuandaa pishi hili
No comments:
Post a Comment