Upishi wa chapati: Mkate wa kusukuma
Vipimo:
- Unga wa ngano mweupe 1 Kilo
- Samli (mafuta) 150gm
- Chumvi 3 vya chai
- Maji ya moto yasichemke lakini Kiasi
- Mafuta Ya Zaituni 4 vijiko vya supu
- Samli tena 200 gms
- Iliki (Hiliki) iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Namna ya kutayarisha na kupika:
(1) Tia
unga kwenye sinia au bakuli kubwa lilo na nafasi, changanya na chumvi,
mafuta ya zaituni, samli 150g, iliki, mimina maji ya moto kwa kipimo cha
kikombe kila unapovuruga unga.
(2) Uunga uwe
mwepesi unapoganda kuwa donge moja kubwa. Uwache kwa muda wa dakika 60
(saa moja hivi) ukiwa umeufinika ili unga ulainike.
(3) Katakata
madonge makubwa yenye ukubwa wa chungwa ili uweze kutoa kila donge
chapati mbili. Ukimaliza hapa weka madonge kwa muda wa nusu saa ukiwa
umefinika bila ya kuingia upepo ndani.
(4) Sukuma
donge ukiwa umelimwagia unga mkavu juu, liwe mviringo. Unaweza kutumia
kifimbo hata chupa kusukumia madonge ikiwa huna kifimbo juu ya meza
au kwenye kibao maalumu cha chapati.
(5) Yayusha
samli nyingine ya 200gm kisha itumie kwa kupaka kwenye kila donge
ukilisukuma duara itakayobakia weka kando utachomea chapatti.
(6) Likate
katikati kwa kidole chako au kijiko upate mgawanyo wa sehemu mbili sasa
kila sehemu utakunja kwanzia ncha moja hadi ikutane na ncha nyengine
kama mkeka, donge lake linakuwa na sampuli, huitwa tabaki
(7) Weka chuma cha kuchomea chapati jikoni moto mdogomdogo.
(8) Sukuma
kila donge kisha mara nyengine mviringo huu utakuwa mviringo wa
kuchoma weka chapati kwenye chuma kavu bila samli iache muda wa dakika
tatu igeuze upande mwengine kisha vilevile , ukiona ina mabapa ya
kuchomeka tia samli ile uloyeyusha kwa kijiko kikubwa kimoja huku
unaizungusha zungusha.
(9) Geuza upande wa pili vile vile mpaka iwive.
(10) Zipange kwenye sahani huku unazifinika, hapa tayari kuliwa kwa mchuzi au mboga yoyote.
Kidokezo:
Ukipenda
kuzichambua kidogo chapati baada ya kumaliza hii unazishika zote kwa
pamoja ikiwa umezikunja, unakunja ngumi au kifimbo kupiga tu mara moja
tosha.
No comments:
Post a Comment