Upishi wa Kebabu
Wapishi wenzangu Asalaam Aleykum kwa cc waislam n Bwana acfiwe kwa upande wa pili.
Haya jongeeni kijiweni tuongezeane ujuzi wa mapishi. Angalia upishi wa KEBABU.
Mahitaji
1. Nyama ya kusaga kl 1
2. Kotmili/giligilani wengine huita kifungu kimoja
3. Kitunguu maji vikubwa vitatu
4. Swaum kikubwa kimoja n tangawizi
5. Mikate ile ya buku miwili ama mitatu
6. Chumvi kiasi
7. Binzali nyembamba na pilipili manga vilivyo sagwa
8. Pili pili hoho kubwa moja
9. Mafuta ya kupikia
10. Ndimu
11. Mayai sita
2. Kotmili/giligilani wengine huita kifungu kimoja
3. Kitunguu maji vikubwa vitatu
4. Swaum kikubwa kimoja n tangawizi
5. Mikate ile ya buku miwili ama mitatu
6. Chumvi kiasi
7. Binzali nyembamba na pilipili manga vilivyo sagwa
8. Pili pili hoho kubwa moja
9. Mafuta ya kupikia
10. Ndimu
11. Mayai sita
Kuandaa
Nyama ya
kababu hua aichemshwi habisa. Kumbuka nyama kama ina maji kumbuka
kuyakamua. Chukua nyama yako weka kwenye chombo kisafi, tia chumvi,
ndimu, unga wa binzari nyembamba na pilipili manga, alafu changanya huo
mchanganyiko wako na uwakikiche umechanganyika vizuri kabisa.
Hatua inayo fuata.
Katakata vitunguu maji katika vipande
vidogo vidogo kama vya sambusa vile, oya kotmili/giligilani zako vizuri
na ukamue maji alafu toa ile mizizi ya nyuma na kisha katakata katika
vipande vidogo vidogo, twanga swaum zako na badala ya hapo tia katika
mchanganyiko wako ule wa nyama. Changanya mpaka uakikiche umechanganyika
vizuri. Kuonja ruksa wapenzi iliuweze jua kama vitu vuote vipo sawa au
laa….
Hatua ya tatu.
Chukua mikate yako toa ile nyama ya
kati nikimaanisha ile nyama ya mkate nyeupe ule upindo wa pembeni ucweke
sababu ni mgumu na co soft. Chambua mikate yako vizuri kabisa na
inyambue nyambue na uweke katika mchanganyiko wako wa nyama, chukua
mayai matatu uweke humo. Changanya vyote sasa kwa pamoja mpaka
uwakikiche vimechanganyika ipasavyo. Na baada ya hapo utafanya kama
unakanda unga wa ngano vilee na upate donge moja takatifu. Utaacha
mchanganyiko wako kwa mda wa kama dk 10 or 15 hivi ili viungo viweze
kukolea kwa uzuri.
Hatua ya nne na mwisho.
Kata vidonge vidodo vidogo ama
upendavyo na kutengeneza style uipendayo, weka kwenye chombo safi,
vyunja mayainyako yale matatu yalio baki na uweke kwenye bakuli toa vile
viini vya ndani na ubaki na ute tu. Weka flampeni/karai lako jikoni na
ucwe na moto mkali, moto uwe wa wastani tu, mafuta yako yakisha pata
moto chukua kebabu zako tosa kwenye ule ute wa yai na uweke kwenye
mafuta yakio jikoni na utarudia kwa vyote viduara ulivyo fanya. Baada ya
hapo vitakua tayari kwa kuliwa. Ni tamuje sasa…..Very yummy waweza
sukum7a na chochote Wallah.
No comments:
Post a Comment