Utamu wa hii cake ni zaidi ya maelezo. Uwepo wa chocolate unaifanya ivutie kwa macho, vanilla inaipa harufu tamu na utamu wake ni zaidi ya muonekano. Ni kitafunwa vizuri wakati wowote ili kuipa familia ladha tamu na mabadiliko.
Kuandaa: dakika 15
Mapishi: dakika 60
Walaji: 8
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Mahitaji
Unga wa ngano vikombe 2
Sukari kikombe 1
Ndizi 2, zilizoiva vizuri
Mayai 2
Mafuta ya kula ½ kikombe (Au butter 2/3 kikombe)
Chumvi kijiko 1 kidogo
Kikombe 1½ cha maziwa
Baking soda kijiko 1 kidogo
½ kikombe cha cocoa ya kuokea (Au chocolate ya unga)
Vanilla flavor kijiko 1 kikubwa
Hii ni keki unayoandaa ukiwa na muda na hamu ya kula kitu kitamu, chenye afya na kinachoweza kukupa furaha. Ni muhimu kuandaa keki kama una muda mwingi wakati wa weekend, ili upate matokeo mazuri zaidi na kujumuika vizuri na familia.
Washa oven weka kwenye nyuzi 350°F (180°C). Acha ipate moto.
Kwenye bakuli kubwa, changanya butter na sukari hadi zichanganyike na kuwa laini. Ongeza mayai, moja baada ya jingine – pasua kisha changanya vizuri.
Kwenye chombo tofauti, changanya unga wa ngano, cocoa, vanilla flavor, baking soda na chumvi. Koroga vizuri. Changanya mchanganyiko huu kwenye bakuli lenye mchanganyiko wa mafuta na sukari. Kwenye chombo tofauti, ponda ndizi hadi zilainike vizuri kisha weka kwenye mchanganyiko wa unga na mafuta. Koroga vizuri.
Ongeza maziwa kidogo kwa wamu kwenye mchanganyiko huku unaendelea kukoroga vizuri. Rudia hadi maziwa yote yachanganyike vizuri.
Paka chombo unachotumia kuokea mafuta na unga vizuri, kisha mimina mchanganyiko kwenye bakuli la kuokea. Weka kwenye oven. Tega oven dakika 45 hadi 50. Jaribu kama cake imeiva – ingiza kijiti au kitu chembamba, kisha toa. Kikitoka kikavu, keki imeiva, kikitoka kimelowa, acha cake kwenye oven kwa muda wa dakika 10 zaidi. Kisha jaribu.
Ukishatoa cake kwenye oven, unaweza kuipaka chocolate juu yake ili ivutie zaidi. Mie sikupaka chocolate, maana uwepo wa chocolate ulikuwa unatosha.
Hii cake unaweza kula kama kitafwa kawaida, muda wowote unapohitaji kutafuna kitu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...
-
Futari ya Mihogo na Viaz Vitamu Kila kitu unapokifanya kwa mfululizo kwa muda mrefu kinachosha. Hata kupika nako kunachosha,i...
-
MAHITAJI/INGREDIENTS Visheti 1.Unga wa Ngano ¼ Kg ¼ Kg Plain Purpose Flour 2.Maziwa ya maji Kikombe Kidogo 1 1 Small Cup...
-
JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...
No comments:
Post a Comment