Saturday 28 October 2017

BAGIA ZA MAHARAGE WAZIJUA???

Image may contain: food

MAHITAJI


MAHARAGE
KITUNGUU MAJI
CHUMVI KIASI
MAFUTA
PILI PILI BOGA
PILIPILI MBUZI
KUANDAA NA KUPIKA
1.Roweka maharage yako hadi yawe laini ,kiasi cha kuweza kusaga kwa kutumia blender , hakikisha maharage hayana makapi .
2.Andaa vitungu na viungo vingine ,kisha katakata saga pamoja na maharage,hakikisha hutii maji mengi katika kusaga ili usipate shida katika uchomaji .
3.Baadaa ya kusaga tia mafuta jikoni katika karai au sufuria ,ukiona yamechemka chukua mchanganyiko wako na anza kuchoma kama uchomavyo kalimati, hakikisha moto hauwi mkali ili bagia zako ziive vizuri .
Pia waweza kutumia aina yoyote ya maharage ama kunde nk. Kikubwa kumbuka havitakiwi kuwa na makapi na usiache kuroweka.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...