Friday 20 October 2017

JIFUNZE KUPIKA VITUMBUA KITAALAMU.

VITUMBUA

 MAHITAJI 

Mchele kikombe (mug) 1 Hamira 1 and 1/ 2 tsp Hiliki 1/2 tsp Sukari 1/2 kikombe Tui la nazi zito 3/4 kikombe about 200 ml Unga wa ngano 2 tblsp Yai 1 Mafuta ya kupikia 

MATAYARISHO 

Loweka mchele usiku mzima angalau masaa 5 au zaidi.weka mchele, hamira, tui la nazi na hiliki kwenye blender saga kwa dakika 5 weka unga wa ngano halafu saga tena mpaka mchele uwe laini.

 Pumzisha blender kila baada ya dakika 3. (unatumia kama dakika 10 mpaka uwe laini). 

Mimina kwenye bakuli weka maji vijiko 2 vikubwa kwenye sukari ikoroge mpaka ichanganyike halafu mimina kwenye batter (mchanganyiko wa mchele).mix vizuri mpaka uhisi sukari imeyayuka.acha batter yako iumuke. Ikisha kuumuka piga yai vizuri (kama hupendi harufu ya yai basi changanya yai na kijiko kimoja cha maziwa hivi inakata harufu). 

Yai likisha kupigika vizuri changanya kwenye batter yako mix vizuri,tayari kwa kuchomwa. Weka chuma kwenye jiko tia mafuta kwenye chuma weka batter yako choma vitumbua kwa moto wa kati ukiona vinaungua punguza moto.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...