Sunday, 15 October 2017

MAPISHI:KIFUNGUA KINYWA CHA VIAZI VITAMU NA CHAPATI ZA MAJI.

Kuna wakati katika leo tena tulikuwa tukipeana ideas namna ya kupangilia kifungua kinywa.Lengo lilikuwa kubadilishana mawazo ili kuondokana na mazoea ya kula kifungua kinywa hicho hicho kila siku.Tunaambiwa mlo wa subuhi ndio unatakiwa kuwa mlo mkubwa kuliko mwingine lakini nyumbani ni tofauti.Chai na mkate wa kwa mangi jioni sahani hiyoo ya ubwabwa na maharage.Kina mama walikuwa wakituma mpangilio wa vitafunywa au namna unavyoweza kuandaa kifungua kinywa kutokana na vyakula vinavyopatikana katika mazingira yetu ya kila siku.
Tuna viazi vitamu hapa
Viazi vitamu sokoni viko tele,mihogo na hata magimbi.
Nikavimenya,nikaviosha na kuvikata hivi kwa sababu mie nilikuwa navikaanga,unaweza pia kuchemsha.
Tayari kuliwa na unaweza kula na kachumbari pia lakini mie sikuweka kachumbari.Sikuishia hapo…


Nikapika chapati za maji,huu ni mkorogo wa unga wa ngano na maji baridi niliweka,mayai manne,iliki na sukari.Niakavikoroga vizuri vyote kwa pamoja.Chapati za maji wapo wanaopenda za chumvi,wengine sukari.Mie napenda zote zote ila hizi zilikuwa za sukari.
Chapati za maji ni mlo rahisi sana kuandaa na fasta,najua kina dada na kina mama karibia wote mnaliweza.
Hapo chapati zipo tayari kuliwa.
Siku sahau matunda tikiti,sasa hivi matunda yapo kibao hasa ya msimu.Kuna mapapai,machungwa,embe,parachichi na matikiti.Tunda la msimu lisikose kwenye kifungua kinywa au tengeneza juisi.
Hapo kifungua kinywa kikawa tayari viazi vya kukaanga,chapati za maji,chai ya maziwa na matunda.
 

N.B Nipo kwenye maandalizi ya jarida la mapishi ya vyakula vilivyopo katika mazingira yetu ya kila siku.Jarida hili limehusisha wanawake na wadada waliopenda kushiriki kutoa ideas za mapishi yao wanayoyajua.Jarida hili la kwanza litagusa kifungua kinywa tu namna ya kupika na namna ya kupangilia huo mlo kwa kuzingatia mlo kamili wenye afya.Lengo hasa ni kumpa mama/dada mawazo kuwa kuna uwanja mpana wa vyakula asikariri.Hata dada wa kazi nyumbani linaweza kumsaidia pia.Mwisho wa mwaka ndio utalipata,tena bure…stay tune

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...