MAHITAJI
Siagi vijiko 6 vya chakula
Chumvi kiasi
Viini vya mayai 2
Baking powder kijiko 1 cha chai
Custard powder kijiko 1 cha chakula
Maziwa ya maji vijiko 4 vya chakula
Unga wa ngano kikombe 1
Yai 1 la kupakia juu
Arki unayopenda(nimetumia vanilla na ya chungwa) kijiko ki1 ki1 cha chai
Ufuta (si lazima)
Sukari kijiko 1 cha chakula (si lazima)
MATAYARISHO
- Kwenye bakuli weka siagi,maziwa,viini ya mayai , baking powder, custard powder, chumvi,arki na sukari
2.Saga kwa kutumia mwiko,mchapo au machine ya kusagia kwa muda wa dakika 3 hadi 5
- Anza kuweka unga wa ngano huku unachanganya
- Unga ukichanganyika ukawa donge , likande kwa dakika 2 hadi 3
- Lifunike,liweke sehem lijivute kwa dakika 7 hadi 10
6.pakaza mafuta trey yako
- Baada ya dakika 7 hadi 10 , lisukume kwa kutumia kifimbo cha chapati mpaka uwe size , isiwe nyembamba sana
8. Kata kwa kutumia kifaa chochote cha kukatia vileja
- Vipange kwenye trey , vipakaze yai juu na ufuta
10 . Vichome kwa oven moto 180°c kwa dakika 10 hadi 15 au mpaka uone vimewiva na kubadilika rangi, vitoe (manjano ilokoza)
*Unaweza kutumia mkaa pia kuokea.
ENJOY NA CHAI AU KAHAWA
No comments:
Post a Comment