Wednesday 29 November 2017

CHAPATI ZA MAJI

CHAPATI ZA MAJI

MAHITAJI

Ngano 1/2 kilo
mayai 3
mafuta au samli 1/4 kikombe
kitunguu kikubwa kilichosagwa 1
Kitunguu Swaumu punje 4
Chumvi 1/2kijiko au kulingana na matakwa yako.

NAMNA YA KUANDAA  chapati za maji
1
Chekecha unga wako vizuri weka katika bakuli safi.
2
Tia maji katika bakuli la unga na ukoroge mpaka upate uji wa wastani si mzito san a wala si mwepesi sana.
3
Ongeza mayai na chunmvi endelea kukoroga.
4
Ongeza kitunguu swaumu na kitunguu maji. Injika kikaango chako jikoni subiri kipate moto. 
5
Chota pawa moja mimina na tandaza kuzunguka kikaango subiri sekunde tano hadi kumi mpaka ikauke kisha geuza upande wa pili.
6
Tia mafuta huku ukigeuza na kuzungusha ili mafuta yaenee pande zote na ili chapati isiungue. Endelea kugeuza mpaka iwe rangi ya kahawia.
7
Hapo chapati zitakua tayari kwa kuliwa.
8
Fanya hivyo kwa chapati zote zilizobakia
Matayarisho hayo yanatosha kupika chapati za mayai/laini sita (6) mpaka kumi (10) . Chapati za maji hupendeza zaidi kuliwa Michuzi mizito, Chai na kadhalika. Nenda kajaribu kuandaa pishi hili


 MAHITAJI 

Ngano 1/2 kilo mayai 3 mafuta au samli 1/4 kikombe kitunguu kikubwa kilichosagwa 1 Kitunguu Swaumu punje 4 Chumvi 1/2kijiko au kulingana na matakwa yako. 


NAMNA YA KUANDAA

chapati za maji 1 Chekecha unga wako vizuri weka katika bakuli safi. 2 Tia maji katika bakuli la unga na ukoroge mpaka upate uji wa wastani si mzito san a wala si mwepesi sana. 3 Ongeza mayai na chunmvi endelea kukoroga. 4 Ongeza kitunguu swaumu na kitunguu maji. Injika kikaango chako jikoni subiri kipate moto. 5 Chota pawa moja mimina na tandaza kuzunguka kikaango subiri sekunde tano hadi kumi mpaka ikauke kisha geuza upande wa pili. 6 Tia mafuta huku ukigeuza na kuzungusha ili mafuta yaenee pande zote na ili chapati isiungue. Endelea kugeuza mpaka iwe rangi ya kahawia. 7 Hapo chapati zitakua tayari kwa kuliwa. 8 Fanya hivyo kwa chapati zote zilizobakia Matayarisho hayo yanatosha kupika chapati za mayai/laini sita (6) mpaka kumi (10) . Chapati za maji hupendeza zaidi kuliwa Michuzi mizito, Chai na kadhalika. Nenda kajaribu kuandaa pishi hili

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...