Wednesday 29 November 2017

CHAPATI ZA KUSUKUMA

CHAPATI ZA KUSUKUMA

MAHITAJI
-Unga wa ngano nusu kilo.
-Siagi vijiko 2.
-Yai moja.
-Chumvi kiasi.
-Hiliki kama unapenda maana wapo ambao ha­wapendi.
-Maji ya uvuguvugu kwa ajili ya kukandia.
-Mafuta ya kupikia.

JINSI YA KUANDAA

Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri.
Mchanganyiko uk­ishachanganyika vizuri weka yale maji ya uvugu­vugu kidogo kidogo huku ukikanda, ukande mpaka uhakikishe haunati ila umekuwa laini.
Kukanda huko kutumie kama dakika 15 hivi ndiyo utalainika vizuri, ukimaliza katakata madonge kulingana na chapati unazotaka, hakikisha saizi inakuwa sawa kwa yote.
Ukimaliza, sukuma donge moja baada ya jingine. Ukishasu­kuma paka mafuta kisha weka donge pembeni mafuta yale yape nafasi ya kuing­ia ili kuifanya chapati iwe laini zaidi.
Ukishamaliza ma­donge yote chukua la kwanza sukuma anza kupika, pika chapati zako kulingana na jinsi ulivyokuwa ukiz­ipaka mafuta moja baada ya nyingine.


 MAHITAJI 

-Unga wa ngano nusu kilo. -Siagi vijiko 2. -Yai moja. -Chumvi kiasi. -Hiliki kama unapenda maana wapo ambao ha­wapendi. -Maji ya uvuguvugu kwa ajili ya kukandia. -Mafuta ya kupikia. 


JINSI YA KUANDAA

 Weka unga wa ngano katika bakuli la kukandia, kisha tia chumvi na hiliki na uchanganye kwanza, baada ya hapo tia siagi na uichanganye vizuri na unga mpaka ipotee. Baada ya hapo tia tena yai na uchanganye vizuri. Mchanganyiko uk­ishachanganyika vizuri weka yale maji ya uvugu­vugu kidogo kidogo huku ukikanda, ukande mpaka uhakikishe haunati ila umekuwa laini. Kukanda huko kutumie kama dakika 15 hivi ndiyo utalainika vizuri, ukimaliza katakata madonge kulingana na chapati unazotaka, hakikisha saizi inakuwa sawa kwa yote. Ukimaliza, sukuma donge moja baada ya jingine. Ukishasu­kuma paka mafuta kisha weka donge pembeni mafuta yale yape nafasi ya kuing­ia ili kuifanya chapati iwe laini zaidi. Ukishamaliza ma­donge yote chukua la kwanza sukuma anza kupika, pika chapati zako kulingana na jinsi ulivyokuwa ukiz­ipaka mafuta moja baada ya nyingine.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...