Thursday 30 November 2017

MAKANDE YA NYAMA

MAKANDE YA NYAMA
Vipimo 
Nyama (kata vipande vidogodogo) - ½ kilo
Maharage - 3 vikombe
Mahindi - 2 vikombe
Kitunguu - 1
Nyanya - 2
Kabichi lililokatwa - 2 vikombe
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chai
Vidonge vya supu - 2
Chumvi - kiasi
Mafuta -1au 2 vijiko vya chakula 
Namna Yakutayarisha
Chemsha mahindi mpaka yawive na maji yakauke kiasi.
Chemsha maharage pembeni nayo mpaka yawive na maji yakaukie kiasi.
Tia mafuta kwenye sufuria anza kukaanga vitunguu , thomu na vidonge vya supu koroga kiasi.
Kisha mimina nyama iliyokatwa vipande acha ikaangike kidogo na chumvi.
Nyama ikishakaangika tia nyanya funika kwa moto mdogo mpaka nyama iwive.
Kisha mimina mahindi na maharage yaliyochemshwa na maji yake kiasi koroga mpaka ichanganyike na mwisho mimina kabichi funikia mpaka kabichi iwive onja chumvi kama imekolea
Halafu malizia kukoroga mpaka ichanganyike na ikaukie kisha pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa.


Vipimo Nyama (kata vipande vidogodogo) - ½ kilo Maharage - 3 vikombe Mahindi - 2 vikombe Kitunguu - 1 Nyanya - 2 Kabichi lililokatwa - 2 vikombe Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chai Vidonge vya supu - 2 Chumvi - kiasi Mafuta -1au 2 vijiko vya chakula 

Namna Yakutayarisha


 Chemsha mahindi mpaka yawive na maji yakauke kiasi. Chemsha maharage pembeni nayo mpaka yawive na maji yakaukie kiasi. Tia mafuta kwenye sufuria anza kukaanga vitunguu , thomu na vidonge vya supu koroga kiasi. Kisha mimina nyama iliyokatwa vipande acha ikaangike kidogo na chumvi. Nyama ikishakaangika tia nyanya funika kwa moto mdogo mpaka nyama iwive. Kisha mimina mahindi na maharage yaliyochemshwa na maji yake kiasi koroga mpaka ichanganyike na mwisho mimina kabichi funikia mpaka kabichi iwive onja chumvi kama imekolea Halafu malizia kukoroga mpaka ichanganyike na ikaukie kisha pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...