Tuesday 19 June 2018

ACHARI YA NDIMU

Ndimu 15, malimau 10
Pilipili mbuzi 3 kubwa,pilipili ya unga 1 tbsp
Fresh garlic paste 3 tbsp
Bizari ya mchuzi 1 tbsp
Chumvi kiasi

Roweka Ndimu kwa maji yamoto hadi maji yapoe, zitoe tumia kitambaa kisafi uzifute maji ziwe kavu zote, zikate mara 2, ziwe vipande 4 kwa kila ndimu 1, zitie kwenye kopo au kidoo, unapozikata zitatoka maji yake pia yatie pamoja na ndimu,

Kwenye kidoo cha ndimu tia ile garlic paste, Bizari ya mchuzi, chumvi na pilipili za kuwasha zikate kate, pilipili ya

Chukua yale malimau yakamue upate juice yke uitie kwenye chupa la ndimu, hakikisha ile juice ya limau imefunika zile ndimu, hapa waweza tumia hata ndimu yenyewe sio lazima limau, au waweza tumia ready made lemon juice, ila fresh lemon au lime ni nzuri zaidi,

Ukimaliza itikise vizuri ichanganyike, au waweza fnannya kwenye bakuli then ukatransfer kwenye kopo. Then ianike kwa jua, kila juice yke ikipungua engeza pamoja na chumvi,

Endelea kuianika mpaka iwive, yaweza take time labda 2 to 3 weeks yategemea na jua itakayopata.

Nimetumia green limes ndio mana nikaziroweka na maji yamoto ili zilainike ila kama utapata ndimu zilowiva za yellow basi waweza skip hiyo process ukaanza na kuzikata moja kwa moja baada ya kuzikosha,

☆kila ukiengeza maji ya limau engeza na vitu vyengine especially chumvi garlic na bizari

TAG NA SHARE NA WENGINE

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...