Tuesday 19 June 2018

CAKE YA CHUNGWA /ORANGE CAKE



Siagi ya kikopo nusu kg 500g

Sukari kikopo 1 (ulichotoa siagi )

Unga kikopo ulotoa siagi  viwili kasrobo (kimoja +nusu yake+robo yake )

Mayai 8 (medium )

Baking powder 1 tbsp

Chungwa 2 za kiasi (maganda na juice yake )

Washa oven 180 c au tayarisha mkaa wa moto  (wa kupambilia)

Saga siagi  na sukari  kwa muda wa dakika 5 mpaka 10 au mpaka uone imeshaanza kuwa nyeupe, anza kutia yai moja moja huku unasaga (hakikisha unasaga vizuri kabla kutia yai jengine ) , endelea na yai la pili usage mpaka unamaliza mayai,

ukimaliza kutia mayai na kusaga vizuri tia baking powder, changanya,

Chukua machungwa uyapare ngozi ya nje yote (tumia grater kupara ili itoke nyembamba na laini sana )

ipare ngozi ya orange yote na utie kwenye mchanganyiko wako na uchanganye vizuri, bakisha kidogo ya kuweka juu ya cake

Punguza speed ya machine yako  (mixer)

Yakate machungwa na ukamue yote kwenye mchanganyiko wako wa cake huku unatia unga kidogo kidogo,  mpaka unamaliza (unga na maji ya machungwa)

Chukua pan au sufuria weka baking paper chini (karatasi ya kupambilia ) ,weka mchanganyiko  na utandaze vizuri, na ubake kama kwa oven moto 180°c , kama kwa mkaa weka moto kiasi kwa muda wa dakika 45-55  inategemea na nguvu ya jiko lako,  ikishawiva iepue wacha ipoe itoe kwenye trey na cake ipo tayari kuliwa ni tam sana ladha na harufu utapenda.

Kabla ya kuepua ichome ujiti mpaka chini kuangalia kama imewiva (kama ujiti una maji maji basi cake haijawiva, kama ujiti mkavu cake imewiva.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...