Sunday 10 June 2018

JINSI YA KUPIKA SAMBUSA ZA NYAMA

Ndugu wapenzi, Leo tunakuja na Jinsi ya
kupika Sambusa Za nyama. Sambusa
Hupendwa na wengi hasa za nyama. Sambusa
ni Tamu sana, wengi hupenda kula pamoja na...
Juisi, soda na hata chai.

Mapishi ya Sambusa Za Nyama /
Jinsi ya kupika sambusa hatua
kwa hatua

Mahitaji
½ kilo Nyama ya iliyosagwa
kijiko 1 kikubwa cha chakula cha Pilipili
manga
Kijiko kimoja cha chakula cha kitunguu
Thomu na tangawizi iliyosagwa
Mafuta ya kupikia Kiasi
Vijiko vinne unga ngano au ute wa yai
kwa kufungia sambusa
Kaki za sambusa/manda/ chapati nyepesi
(unaweza kununua zilizokuwa tayari
zimeshakatwa kwa ajili ya sambusa au
kama utanunua zile sheet pana utazikata
kwa inchi 4 upana wa ruler yaani upate
mistari 3

Directions
1. Kausha nyama ya kusaga kwa kitunguu
swaumu (thomu) na tangawizi pamoja na
chumvi mpaka ikauke vizuri Iwache ipoe.

2. Kata kata majani ya kotmiri weka
upande Kata kata upate vipande vidogo
vidogo(chop) vya vitunguu maji.

3. Zikate pili pili zako slice za mviringo
vidogo vidogo.

4. Wakati ukimaliza matayarisho haya na
nyama yako itakuwa ishapoa kabisa hapo
ndio utachanganya,bizari nzima pamoja na
pilipili manga pamoja na vitu vyote
ulivyokwisha vitayarisha

5. Koroga unga ndani ya kibakuli au ute
wa yai
6. Weka kaki kwa mfungo wa triangle
yaani pembe tatu kama kofia na

7. weka mchanganyiko wa nyama yako
kiasi na uanze kuzifunga sambusa zako na
ukifika mwisho hapo ndipo upake unga
wako kwa ajili ya kuifunga isifunguke
wakati wa kuchoma, pendelea kutumia
kaki 2 kwa kila sambusa moja.

8. Kuchoma kwake ikiwa unazifanya na
kuzichovya hapo hapo mafuta lazima yawe
baridi (ninakusudia uweke mafuta na uzitie
sambusa kabla hayajapata moto).

9. Na ikiwa uliziweka kwenye friji
zikaganda basi unatakiwa uzichome kwa
mafuta ya moto

KIDIKEZO
Watu wengi hupata usumbufu katika kufunga
sambusa, Jaribu mara kwa mara utafanikiwa
tu, ni kiasi cha kuzowesha mikono kufuatisha
ile Triangle tu.
Pia waweza kutupia njegere kiasi zilizopikwa
katika mchanganyiko wako wa nyama ili
kupendezesha zaidi.
Hivyo ndivyo Jinsi ya kupika Sambusa za
nyama

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...