Sunday 10 June 2018

WALI WA BIRIANI

Mchele kilo 1
Nyama kilo 1
Samli ½ kilo
Mbatata ½ kilo
Vitunguu maji kilo 1
Thomu gram 150
Tangawizi mbichi gram 150
Hiliki gram 50...
Mdalasini gram 100
Mtindi painti 1
Siki kiasi
Majani ya nanaa fungu moja
Chumvi kiasi
Zaafarani kidogo (irowekwe kwa maji ya moto
nusu kikombe cha kahawa)
Tungule ilosagwa
Tungule ya kopo

1 Menya vitunguu maji uvioshe
uvikate. teleka sufuria utie samli, ikichemka tia
vitunguu uvikaange bila ya kuvivuruga mpaka
viwe vyekundu. Vichuje uvitoe halafu vitandaze
katika sinia.

2 Twanga mdalasini na hiliki mpaka
viwe laini kama unga. Menya thomu uitwange
pamoja na tangawizi mbichi.

3 Kata nyama vipande vikubwa kisha
tia chumvi na vitu ulivyovisaga (yaani tangawizi
mbichi na thomu) vile vile tia unga unga wa
mdalasini na hiliki pamoja na mtindi wa maji.
Pika mpaka karibu nyama kuiva kabisa ndipo
utie mbatata. Ukiona mbatata zimeshaiva tia
siki.Usiache kukauka kabisa, bakiza rojorojo.
Tia maji katika sufuria na chumvi yakichemka tia
mchele. Acha utokote, angalia kiini cha wali
ukiona umeshaiva uchuje.

4 Angalia sufuria ya nyama na rojo
lake lisiwe limekauka kabisa, lazima ziwe na
maji kidogo. Chukua vile vitunguu
ulivyovikaanga vikapoa uvinyunyuzie juu ya
masalo yote (usikoroge). Halafu utie mchele
uliouchuja, nyunyuzia maji ya zaafarani juu ya
wali wote halafu unyunyuzie samli ile uliyochuja
kutoka kwenye vitunguu ulivyovikaanga ienee
juu ya wali wote. Kisha funika upalie makaa.

5 Wali ukishakuwa tayari utaupakua.
lakini unapotaka kuupakua lazima kwanza
uutoe wali wote mweupe uutie katika chombo
chengine, halafu uyakoroge masalo
yachanganyike sawasawa kisha ndio uyatie juu
ya wali katika kila sahani

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...