Sunday 24 June 2018

JINSI YA KUTENGENEZA BARAFU ZA MAZIWA.



MAHITAJI

(kwa mahitaji haya utatoa zaidi ya pisi 200 za barafu ukitumia vifuko vya size 1¼ X 10)
Maji lita 7
Maziwa ya unga 1 cup (brand yoyote)
Unga wa wanga (corn starch) 2 cups uchanganye na maji lita 1.5 (unga wa wanga unauzwa supermarket) au sokoni unga wa ubuyu
Sukari kilo 1¾ (waweza punguza)
Chumvi ½tsp (ukipenda)
Utaweka ladha uipendayo (vanilla, mango, chocolate, pineapple, nk) Mifuko 300 ya kufungia ice candy (mifuko ya barafu)
HATUA:
1. Weka maji lita 7 kwenye sufuria kubwa na weka jikon yachemke, ongeza sukari na chumvi(ukipenda), kisha changanya vizuri hadi viyeyukie humo .
2. Ongeza ile corn starch na maziwa ya unga kwenye hayo maji yanayochemka, koroga vzr ili kusitokee mabujabuja, chemsha kwa dk 8, kisha zima jiko, acha ipoe kwa saa kadhaa kisha ongeza ladha uipendayo.
3. Funga kwenye vile vifuko na gandisha hadi ziwe barafu.

Baada ya kugandisha..... what next...

Tayari kwa kula au kuuza(sh 50 au sh 100,200,500 kulingana na kiwango ulichojipangia)

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...