Wednesday 20 June 2018

KASHATA ZA MAZIWA YA UNGA (Swahili)


MAHITAJI

Maziwa ya unga kikombe 1 na nusu

Sukari kikombe 1 na robo

Maji kikombe 1 na nusu

Arki ya vanilla kijiko 1 cha kula

Rangi ya chakula kjk 1 cha kul(orange)

Mafuta ya kupikia vjk 2 vya kula

MATAYARISHO

Kwenye sufuria au pan tia maji na sukari , wacha ichemke
Ikianza kutoa mapovu mazito ( dakika 8 hadi 10) tia rangi , arki na mafuta ya kupikia , koroga kg wacha ichemke tena

Subiria tena kwa dakika 3 mpaka 5 au iwe nzito ukiigusa kwa vidole viwili ukiwachia ifanye kama uzi au mfano wa gundi

Tia maziwa ya unga koroga haraka haraka kwa dkk 1 au mpaka mchanganyiko uwe mzito


Pakaza mafuta sehem yako ya kukatia au trey , weka mchanganyiko wako, tumia mwiko,kijiko au kifimbo kuwekea sawa,  wacha upoe na ukate shape unayopenda

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...