Friday 22 June 2018

MIKATE YA BWANA

image
MAHITAJI
Unga wa ngano vikombe 3
Siagi vijiko 2 vya supu
Baking powder kijiko 1 cha supu
Hamira kijiko 1 cha supu
Sukari vijiko 2 vya supu
Chumvi kiasi
Tui la maji kikombe 1
Maji
Maziwa ya unga vijiko 5 vya supu
Ufuta
Yai 1
MATAYARISHO
1 . Kwenye bakuli changanya unga wa ngano,maziwa ya unga na baking powder changanya vizuri
2. Kwenye kibakuli chengine kidogo tia maji ya uvugu uvugu vijiko nusu kikombe tia hamira iwache kwa dakika 5 ,tia sukari ,chumvi, yayusha siagi utie koroga sukari iyayuke
3.Anza kutia unga wa ngano huku unachanganya na tui la maji mpaka donge lishikane , engeza maji yakihitajika
4. kanda  unga mpaka uwe laini na haugandi kwenye vidole ugawe madonge 3 mpaka 4,yafanye duara yawache yaumuke sehem ya joto
5. Tumia kifimbo  sukuma donge la unga(kama chapati)  lisiwe jembamba sana, paka mafuta kunja na uzungushe  kuanzia mwanzo mpaka mwisho kama unavyofanya chapati uweke pembeni ziumuke tena.
image
  6. Zikishaumuka sukuma duara ya size nzuri isiwe nyembamba ,weka kwenye trey paka yai juu uweke ufuta na uchome (ubake) oven 180°c kwa dakika 15 mpaka 20 au mpaka iwive na upige rangi ya light brown  , itoe kwenye trey,  choma mpaka yote inamaliza na ipo tayari kuliwa.
image

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...