Thursday 7 June 2018

Ndizi za kuunga na nazi






Mahitaji

  • Ndizi mbichi 6
  • Nazi 1
  • Vitunguu 2
  • Pilipili hoho 1
  • Karoti 2
  • Nyanya 3
  • Chumvi kijiko 1 kikubwa

Maelekezo

  • Menya ndizi kisha ziweke kwenye maji. Hii inasaidia kutopata weusi na utomvu unaotokana na kutokuwa kwenye maji. Kisha osha ndizi zako na uweke tena kwenye chombo chenye maji mengi.
  • Menya vitunguu na kisha katakata vipande vidogo.
  • Kata pilipili hoho, menya nyanya uzikate vipande.
  • Kata karoti na nyingine kwangua maganda.
  • Andaa nazi kwa kuikuna na kukamua tui 2 – moja tui zito weka kwenye chombo pembeni na tui jepesi kwenye chombo tofauti.
  • Bandika chungu au sufuria ya kupikia jikoni. Ongeza tui zito kidogo, acha lichemke mpaka litoe mafuta.
  • Tui likishatoa mafuta, weka vitunguu vyako mpaka vikaribie kuiva halafu ongeza pilipili hoho. Koroga kiasi halafu weka karoti. Endelea kukoroga mchanganyiko kwa dakika 2 halafu ongeza nyanya kwenye sufuria. Ongeza chumvi na kisha funika sufuria na mfuniko hadi nyanya ziive (takribani dakika 5 hadi 8).
  • Nyanya zikiiva, ongeza ndizi kwenye sufuria yenye viungo. Endelea kukoroga.
  • Ongeza tui jepesi kwenye sufuria yenye ndizi huku unaendelea koroga ili tui lisikatike.
  • Ikishachemka, ongeza na kupungua tui, ongeza tui zito huku ukiendelea koroga mpaka lichemke.
  • Acha mchanganyiko uchemke kwa takribani dakika 10 ili tui liive.
  • Ndizi zako zitakua zimeiva.
Jirambee na ladha ya maisha..! Enjoy ndizi za kupika.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...