Thursday 7 June 2018

Tambi za nazi, njegere, hiliki na sukari





Mahitaji

  • Nazi
  • Tambi (Soma kwa makini muda ulioshauriwa kuzichemsha tambi kwenye paketi)
  • Hiliki
  • Sukari
  • Njegere 1/4 kilo


Maelekezo

  • Tayarisha njegere kwa kuziosha na kuzichemsha hadi ziive.
  • Kuna nazi, kamua tui zito tu.
  • Menya hiliki kisha zitwange kwenye kinu.
  • Bandika maji jikoni. Yakichemka tumbukiza tambi.
  • Toa tambi kwenye maji dakika moja pungufu ya muda ulioshauriwa. Hii inasaidia kufanya tambi ziwe ngumu ili kuweza kuiva vizuri ukipika na tui.
  • Weka tambi kwenye chujio ili zitoe maji.
  • Bandika tui jikoni. Weka hiliki. Koroga mchanganyiko ili kupata tui laini na kuzuia lisikatike.
  • Weka njegere kwenye tui. Koroga ili ziweze kuchanganyika. Ni vizuri kama utaponda njegere ili kupata rojo tamu kwenye mchanganyiko.
  • Tui likishachemka weka tambi na sukari huku ukiendelea kukoroga taratibu hadi tui likauke na kubaki mafuta.
  • Chakula kipo tayari kuliwa

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...