Monday 2 July 2018

Jinsi ya kupika biryani ya kuku, ng'ombe au mbuzi


Jinsi ya kupika biryani ya kuku, ng'ombe au mbuzi

[​IMG]

Mahitaji

  • 1 kilo mchele wa basmati mrefu
  • 1 kilo nyama iwe ya kuku au ng'ombe au mbuzi kata katika umbo dogo la kutosha kula kisha ichemshe na tangawizi na kitunguu swaumu, unga wa binzari (turmeric powder) pili pili manga na chumvi ili kuweka ladha nzuri. Ikisha iva itoe iweke pembeni na mchuzi wake uweke pembeni utautumia baadae.
  • 1 kilo ya vitunguu kata slice ( mviringo)
  • 1 kilo nyanya nyekudu zilizoiva, osha vizuri kisha katakata saizi ndogo ndogo sana
  • 240 ml ya samli au mafuta yeyote ya kupikia
  • 2 maggi chicken soup cubes
  • 3 kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili mwekundu
  • 1/2 kijiko kidogo cha chai unga wa binzari (turmeric powder)
  • 3 kijiko kidogo cha chai unga wa girigilani (coriander powder)
  • 2 kijiko kikubwa cha chakula mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu swaumu vilivyosagwa (ginger-garlic paste )
  • 50 gram korosho iliyo kaangwa usizisage zibaki nzima
  • 50 gram majani ya girigilani (fresh coriander leaves, washed and chopped)
  • 8-12 mbegu za nzima ya hiriki (green cardamoms)
  • 4 bay leaves ( sifahamu kiswahili chake)
  • 15 mbegu nzima ya pili pili manga (whole black peppercorns)
  • 30 gram majani mabichi ya minti ( mint leaves )
  • Chumvi kulingana na mahitaji yako

Jinsi ya kupika

  1. Weka mafuta katika sufuria yako iliyokwisha pata moto, kisha kaanga nyama yako iliyokwisha chemshwa mpaka iwe na rangi ya kahawia.
  2. Kisha itoe nyama hiyo na ichuje mafuta na mafuta yanayobaki weka kitunguu na endelea kukaanga kwa dakika 7-10 kisha weka unga wa binzali, unga wa pili pili mwekundu, unga wa girigilani, bay leaves, mbegu za hiliki na nusu ya mbegu za pili pili manga.
  3. Changanya vizuri mpaka utapata mchanganyiko mzuri mkavu miminia humo maji uliyotunza baada ya kuchemshia ile nyama yako na kuiweka pembeni ipoe. kisha weka nyanya fresh ndani ya sufuria yako pika mpaka maji yakauke na mafuta yaanze kuoneka kwa juu ndani ya sufuria.
  4. Kisha weka nyama yako ndani ya sufuria pole pole halafu punguza moto acha ijipike kwa muda mpaka mchuzi wako na nyama viwe na ladha pia usisahau kuweka chumvi kulingana na ladha unayopenda.
  5. Chukua sufuria nyingine weka mafuta ya samli na vitunguu kisha kaanga na majani ya girigilani, majani ya mint na korosho kisha funika kwa dakika 10.
  6. Weka wali wako mkavu uliokwisha oshwa vizuri na uchanganye vizuri. Ongeza vikombe 5 vya maji na chumvi kidogo. M
  7. Mchele ukishaanza kuchemka funika sufuria lako na punguza moto. Maji yakisha kauka kiasi weka mchanganyiko wa ile nyama yako nusu tu juu ya wali wa basmati na acha wali uive kabisa kisha utakua tayari kupakua na kula chakula chako kikiwa cha moto.

No comments:

Post a Comment

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO

JIFUNZE KUTENGENEZA TAMBI KWA MTINDO WA KIMOROKO TAMBI HIZI NI MAARUFU SANA NCHINI MOROKO, NI RAHISI KUANDAA NA NI TAMU SANA KWA...